Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo Taifa LetuHotubaHotuba za Marais Alh.Ali H. Mwinyi

Mheshimiwa Alhaj  Ali Hassan Mwinyi alikuwa rais wa pili wa Tanzania ,aliongoza serikali ya awamu ya pili kuanzia tarehe 5 Novemba 1985 hadi Novemba 1995. Mheshimiwa Alhaj Ali Hassan Mwinyi alizaliwa tarehe 5 Mei, 1925 Kivule, Mkuranga,  mkoa wa Pwani. Alipata elimu ya msingi na sekondari  katika shule za Mangapwani na Dole kati ya  1933 na 1942 Zanzibar.

Kitaaluma mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi ni mwalimu mwenye diploma kutoka Chuo Kikuu cha Elimu ya watu wazima Dublin , Uingereza, mwaka 1954-1956. Aidha alikuwa mwalimu wa shule za msingi za Mangapwani na Bumbwini, Zanzibar. Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi pia ana cheti cha umahiri wa lugha ya kiingereza, alichohitimu katika taasisi ya Regent, Uingereza mwaka 1960 na cheti cha umahiri wa lugha ya kiarabu alichohitimu, Cairo, Misri, mwaka 1972-74.

Kisiasa, mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi alijiunga na chama cha Afro Shiraz(ASP) mwaka 1964 na kushika nyadhifa mbalimbali za serikali ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama vile Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu Zanzibar 1963, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1970 na kati ya mwaka 1982 hadi 1983 alikuwa Waziri wa Afya, Wizara ya Mambo ya Ndani, Maliasili na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Misri.

Mwaka 1983 alichaguliwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais na mwaka 1984 alichaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sehemu hii inakuletea baadhi ya hotuba alizotoa wakati wa uongozi wake.  

 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-21 19:15:02
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0